Sheria na Masharti
- Mchezo wa kubashiri utakuwa wazi kwa washiriki ambao wana miaka kumi na nane na zaidi na ambao ni wakazi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Waandaaji wana haki ya kuhoji uhalali wa miaka kutoka kwa washiriki na wanaweza kukataa ushiriki na kutoa zawadi kwa watu wanaoshindwa kutoa ushahidi wa uhalali huo
- Watu wote wa kawaida (mbali na watu wale walioajiriwa na watayarishaji kwa kipindi chote cha mchezo na vilevile jamaa zao wa karibu na wenza wao) wanaruhusiwa kushiriki kwenye mchezo wa kubashiri.
- Ushiriki kwenye mchezo huu wa kubashiri utaruhusu kutangazwa kwenye jamii, kutuma kwa taarifa kwa wengine, kutuma tena, kutengeneza vitu vingine kutokana na picha au machapisho ya filamu, picha, picha za kupiga, sauti na/au data binafsi za mshindi kwa ujumla au kwa namna yoyote ya mawasiliano kwa ajili ya madhumuni yoyote wakati wa kampeni na hadi mwaka mmoja wa kumalizika kwa kampeni hii. Mshiriki hastahili kulalamikia hasara yoyote au fidia kwa namna yoyote kwa sababu ya kifungu hiki kinapotekelezwa.
- Mwendesha ubashiri ana haki ya kuhakiki uhalali wa washiriki wote na kumuondosha mshiriki yeyote kwa sababu zozote hasa pale ambapo kuna sababu za msingi za kuamini kuwa mshiriki amekiuka moja kati ya vigezo na masharti haya.
- Ikitokea kuwa mshiriki yeyote ameondoshwa kwenye mchezo wa kubashiri, hataruhusiwa kushiriki kwa namna yoyote kwenye mchezo kwa kipindi chote cha mchezo. Hata hivyo, kulingana na kukubali kwake na kukiri kukiuka vigezo na masharti haya, mwendesha mchezo wa kubashiri anaweza kumsamehe na kumkubali na kumpa nafasi nyingine ya kushiriki kwenye kubashiri.
- Kwa kushiriki kwenye mchezo wa kubashiri, mshindi anakubali kuwa taarifa zao zozote ikiwemo, majina, majina ya ukoo, picha, na picha za video zinaweza kutumika na mwendeshaji kwa sababu za kimatangazo bila ya kuomba ridhaa ya awali ya mshindi na bila malipo.
- Fedha/zawadi zote lazima zichukuliwe katika kipindi cha siku 30 kuanzia tarehe ya matangazo ya awali ya mshindi.
- Zawadi yoyote ambayo haikuombwa na mshindi itapelekwa na kujumuishwa kwenye fedha za taarifa ya mwaka
- Mwendesha mchezo wa kubashiri anakubali kuwa hakuna majukumu kwa namna yoyote kwa ajili, kujumuisha bila ukomo wa, kosa lolote, kufuta, mwingiliano, hitilafu, kuchelewa kwenye uendeshaji au usambazaji, kukosekana kwa mawasilano wakati yanapokwa hayapo katika hali ya kawaida au yamekatika
- Kila mshiriki,kwa kucheza mchezo wa kubashiri anakuwa makini,mwangalifu na mwenye akili timamu kwa muda wote kwa kipindi cha kucheza mchezo wa kubashiri. Hakuna mazingira ya uzembe wa namna yoyote na ya kiasi kikubwa ya mshiriki yanayoweza kumhusisha mwendeshaji. Kwa kushiriki kwenye mchezo,washiriki wanaoingia kwenye mchezo wanakubali kuwa taarifa zote zilizowasilishwa ni za kweli, ni za hivi karibuni na zimekamilika.
- Kila mshiriki anakubali kuwa amesoma na kuelewa vigezo na masharti haya na kwa kukubaliana na njia zilizotolewa, mshiriki anaashiria kukubali moja kwa moja na kuelewa kwa ukamilifu vigezo na masharti haya na kukubali kupokea mawasiliano ya meseji kutoka kwa mwendeshaji au yeyote anayehusiana nao kwenye kwenye simu zao kuhusiana na mchezo wa kubashiri, kupokea mawasiliano ya simu au ofa ya matangazo kutoka kwa waendeshaji au jamaa zao/wanaohusiana nao.
- Waendeshaji wana haki ya kufuta, kubadilisha au kurekebisha vigezo na masharti haya muda wowote na mshiriki atajulishwa kwa njia yoyote mwafaka ya mawasiliano
- Ikitokea migogoro inayohusiana vigezo na masharti au matatizo yanayohusiana na bahati nasibu,uamuzi wa mwendesha mchezo atakata rufaa kwenye Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania na baada ya hapo, hakuna mawasiliano ya kina au majadiliano yatayokubalika
- Mwendesha mchezo ana haki ya kuamua namna na jinsi ya kuwapata washindi.
- Majina ya washindi yanaweza kuchapishwa kwenye gazeti lolote au kutangazwa kwenye vyombo vya habari bila kuomba ridhaa ya mshindi.
- Ikitokea migogoro inayohusiana vigezo na masharti au matatizo yanayohusiana na kutangaza mchezo, uamuzi wa muandaaji wa mchezo utakuwa ndio wa mwisho na hakuna mawasiliano au majadiliano yatayokubalika
- Makubaliano haya kati ya muandaaji na mshiriki yatabaki kwa namna yalivyo na yataanza wakati muandaaji anapotoa ofa (usihesabu ofa inapotokea kuna uahirishaji wa muda kwa sababu za kiuendeshaji kama kufanya ukarabati, matengezo yaliyopangwa kufanyika na kuhuisha miundombinu.
- Taarifa kuhusu idadi ya wanaoingia (washiriki/nafasi) alizopata mshiriki wakati wa kutangaza mchezo zitatumwa kwa mshiriki kwa meseji moja kwa moja baada ya kupokea kila meseji kutoka kwa muandaaji.
- Zawadi za kubashiri
- Zawadi za kila siku
- Zawadi za kila siku zitakuwa zinatolewa papo kwa hapo kila siku kuanzia Jumatatu hadi Jumapili.Kila mshindi atapokea taarifa kwa meseji ya ushindi wa zawadi na zawadi ya fedha itawekwa moja kwa moja kwenye akaunti yake ya simu. Wachezaji wa kila siku wanaweza kufanya miamala mingi ya mchezo kwa siku
- Zawadi ya Bonasi Mshindi wa bonasi anaamuliwa kulingana na tangazo/maelekezo ya bonasi.Mshindi atataarifiwa ama kwa meseji au kupigiwa simu kutoka kutoka namba ya simu ya kampuni iliyoidhinishwa.
Vikomo vya Kubashiri na Malipo
Kiwango cha chini cha kubashiri ni TZS 500Kiwango cha juu cha kubashiri ni TZS 200,000
Kiwango cha juu cha ushindi kwa kila bet ni TZS 3,000,000
Ushindi wa jumla kwa mteja mmoja (ukitoa jackpot) kwa siku hautazidi TZS 10,000,000
Ushindi wa jumla kwa mteja mmoja kwa wiki hautazidi TZS 70,000,000
Ushindi wa jumla kwa mteja mmoja kwa mwezi hautazidi TZS 280,000,000
Kiwango cha juu kwa mteja mmoja kutoa salio kwa siku ni TZS 1,000,000
Kiwango cha juu kwa mteja mmoja kutoa salio kwa wiki ni TZS 7,000,000
Kiwango cha juu kwa mteja mmoja kutoa salio kwa mwezi ni TZS 28,000,000